Bodi ya Mikopo ya WanafunzI wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2019/2020ikiwa ni maandalizi ya kukaribisha maombi ya mikopo kwa mwaka ujao wa masomo wa 2019/2020.
Mwongozo huo wa kina unataja sifa za waombaji, utaratibu wa kuomba mikopo, na melekezo mengine muhimu, na unapatikana kwenye tovuti hii.
- KUPAKUA MUONGOZO KWA KISWAHILI: BOFYA HAPA
- GUIDELINES AND CRITERIA IN ENGLISH : CLICK HERE
HESLB inatarajia kuanza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia Juni 15, 2019 hadi Agosti 15, 2019, ikiwa imetenga kipindi cha majuma mawili kuwapa fursa waombaji wa mikopo watarajiwa kusoma kwa makini mwongozo huo na kujiandaa kuomba mikopo.
Aidha, HESLB inawakumbusha wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya shahada ya kwanza kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kuwa na nakala za vyeti vifuatavyo vilivyothibitishwa na Wakili, Hakimu:
- Cheti cha Kidato cha Nne;
- Cheti cha Kidato cha Sita;
- Cheti cha Stashahada (Diploma);
- Cheti cha kuzaliwa
- Cheti cha kifo cha mzazi au wazazi.
Nakala za vyeti (d na e) ziwe zimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar.
- Aidha, Wanafunzi wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu wanapaswa kuwa na barua zinazothibitisha ulemavu huo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa, Wilaya au Kituo cha Afya cha Serikali;
- Wanafunzi ambao walifadhiliwa masomo yao katika ngazi ya Sekondari au Stashahada (Diploma) wawe na barua za uthibitisho wa udhamini huo kutoka katika taasisi zilizogharamia masomo yao;
- Waombaji wote wa mikopo wanakumbushwa kuusoma kwa makini mwongozo wa 2019/2020 na kuuzingatia.
No comments:
Post a Comment